Zaidi ya watu 30 wapoteza maisha katika moto Ukraine ,PICHA NA VIDEO
Watu thelathini wamepoteza maisha katika moto uliowaka katika jengo mjini Odess.
Zaidi ya watu thelathini wameuawa katika tukio la kiuhalifu huko mji wa Odessa kusini mwa Ukraine,wakati huu vurugu zikienea nchini humo na kuwa siku ya hatari zaidi tangu serikali ya Kiev inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi ishike madaraka.
Kwa
mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Ukrane ni kuwa takribani watu 31
walipoteza maisha ijumaa kwa kuungua moto,huku vyombo vya habari nchini
humo vikiarifu kuwa makundi ya watu wanaounga mkono Urusi waaminika
kuwepo katika jengo lililokuwa likiungua.
Wengi wa
waliopoteza maisha walikosa hewa safi na kujikuta katikati ya moshi
mkali wakati wengine wakipoteza maisha wakijitahidi kujiokoa kwa kuruka
kupitia madirishani.
Wizara ya
mambo ya kigeni ya Urusi imetoa wito kwa Ukraine na mataifa ya
magharibi kuwajibika na kukomesha uharibifu dhidi ya waukraine huku
ikilaumu Kiev kutowajibika kudhibiti uhalifu.
Hata
hivyo Hapo jana Serikali ya Ukraine ilizindua operesheni ya kijeshi
kuwasaka na kuwaondoa waasi wanaoiunga mkono serikali ya Urusi, na ambao
wanadhibiti majengo ya serikali mashariki mwa nchi hiyo.
Operesheni
hiyo imeanzia katika mji wa Slaviansk, ambao waasi wamekuwa
wakikabiliana na maafisa wa usalama kwa wiki kadhaa sasa katika
shinikizo la kuwataka waondoka katika mji huo.
0 comments:
Post a Comment