Posho mpya zilizoongezwa kwa Wabunge
Baada
ya kuhairishwa kwa Bunge la maalum la Katiba,Bunge la bajeti limeanza
Mei 06 Dodoma ambapo wabunge kuanza kulipwa viwango vipya vya posho
ambapo itakua ni shilingi 300,000 kwa siku ambayo ni sawa na viwango
sawa na walivyokuwa wakilipwa wajumbe bunge maalum la katiba.
Kabla
ya kupandishwa kwa posho hizo Wabunge walikua wakilipwa 200,000 kwa
siku ambayo mgawanyo wake ulikua ni sawa na 70,000 kama posho ya
kikao,80,000 posho ya kujikimu na 50,000 gharama za usafiri,nyongeza
hiyo ya kila mbunge ambayo ni nyongeza sawa na asimilia 50 litaigharimu
Bunge la Jamhuri ya Muungano kiasi cha Tsh Bilioni 18.5 kwa siku 52
zilizotengwa kwa ajili ya bunge hilo la bajeti.
Bunge hili linategemea kumalizika June 27.
0 comments:
Post a Comment