Akiingizwa kwenye gari la wagonjwa tayari kwa kupelekwa hospitali kwa hatua zaidi
Akiingizwa kwenye gari la wagonjwa tayari kwa kupelekwa hospitali kwa hatua zaidi
Mmoja
wa watu aliokuwa nao ambaye yaelekea ni mfanyakazi mwenzake akiwa
anaingia katika gari hilo huku akiwa amebeba nguo na viatu vya Rashid
John Chilwangwa
Gari la wagonjwa lililombeba likiondoka uwanjani kuelekea hospitali.
Na Mwandishi Wetu
MAADHIMISHO ya
Siku ya Wafanyakazi Kitaifa, maarufu kama Mei Mosi yaliyofanyika leo
jijini Dar es Salaam yameingia dosari baada ya mmoja wa wafanyakazi
kufariki dunia uwanjani kwa ghafla akiwa katika maadhimisho hayo.
Mfanyakazi
huyo anayedaiwa kufanyakazi Ikulu alizidiwa ghafla akiwa katika
maandamano na kupatiwa huduma za kwanza lakini hali yake ilizidi kuwa
mbaya na hatimaye kudaiwa kupoteza maisha akipatiwa huduma na madaktari
na wahudumu kutoka kikosi cha msalaba mwekundu waliyokuwa katika
maadhimisho hayo.
Thehabari.com
ilishuhudia mfanyakazi huyo akiletwa katika kambi ya watu wa huduma ya
kwanza iliyokuwa katikati ya uwanja wa Uhuru, kisha kupatiwa huduma ya
kwanza bila mafanikio na baadaye alifariki dunia. Kwa mujibu wa taarifa
kutoka katika kundi ambalo lilimleta mfanyakazi huyo baada ya kuzidiwa
ghafla lilimtaja kuwa jina lake ni Rashid John Chilwangwa.
Mmoja
wa wafanyakazi waliyokuwa wameandamana na mfanyakazi huyo ambaye
hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa yeye si msemaji akisimulia tukio
hilo, alisema John Chilwangwa (45) walikuwa naye katika sherehe za
maadhimisho na hali yake ilibadilika kabla ya kuingia uwanjani na
aliomba aende kujisaidia haja ndogo baada ya hapo alianza kuishiwa
nguvu.
“…Si
tulishangaa alikaa muda kidogo akijisaidia baada ya kumfuata tulimkuta
ametoka ndani ya choo na kuja nje na kisha kukaa kwenye tofali huku
akisema anajisikia kuishiwa nguvu na hali ilibadilika ndo tukamleta
hapa,” alisema shuhuda huyo.
Alipoulizwa
hali yake kwa sasa ambapo alikuwa ameingizwa kwenye hema la huduma ya
kwanza kwa wahudumu kutoka kikosi cha msalaba na madaktari alisema
wamejaribu kumuhudumia lakini bahati mbaya amefariki dunia tayari.
“…Tumeambiwa na madaktari kuwa ameshafariki tayari,” alisema shuhuda
huyo ambaye alikuja na mgonjwa huyo.
Mwandishi
wa habari hizi alishuhudia madaktari wakijaribu kumtundikia dripu huku
wakijaribu kurudisha mapigo ya moyo kwa kushtua mara kadhaa lakini
juhudi ambazo hazikuzaa matunda. Baada ya kubaini amefariki dunia
walisita kumwekea dripu ambayo ilikuwa inaandaliwa na badaye walimfunika
kwa shuka nyeupe na kuita gari la wagonjwa tayari kwa kumpeleka
hospitali kwa uchunguzi zaidi. Hata hivyo hakupatikana mara moja daktari
kuzungumzia kilichomsibu Chilwangwa.
0 comments:
Post a Comment