TAPELI AKAMATWA BUNGENI ,ANGALIA PICHA
Tapeli huyu amekuwa akidanganya Madreva wa Wabunge kuwa yeye ni Dreva wa TASAF amekwama Dodoma anahitaji Msaada waKifedha,Amekuwa
akioneakana Viwanja nje ya Bunge tangu Bunge la Katiba akiwalaghai Watu
Mbalimbali kuwa yeye ni Dreva na wakati Mwingine akihusika na Utapeli
wa Kujiita Dalali wa Viwanja hapa Dodoma.
Akiwa Chini ya Ulinzi Mkali.
Akipandishwa kwenye Gari la Polisi kupelekwa Kituoni kwa hatua zaidi za Kisheria.
Kijana
Mmoja aliyefahamika kwa jina la Ally Mwinyi na Kujitambulisha anatokea
VIKINDU-Pwani amekamatwa na Jeshi la polisi kwa Ushirikiano na Madreva
wa Wabunge hapa Dodoma kwa tabia yake Mbaya ya Kutapeli watu.
Kijana
huyo amekuwa akijihusisha na Matukio Mbalimbali ya Utapeli hapa Dodoma
kwa nyakati tofauti na kwanji tofauti na kwa watu tofauti.Utapeli wake
amekua akiufanya kwenye Uuzaji wa Viwanja akijidai yeye ni Dalali wa
Viwanja,Pia amekamatwa akiwa na Fungo “FAKE” za Gari ambazo amekuwa
akitumia kutembea nazo na kujidai yeye ni Dreva wa TASAF amekwama Dodoma
hivyo anahitaji Msaada,Kwa nyakati tofauti Madreva wamekuwa wakikutana
naye na kuwaomba masaada na hatimaye Kupewa fedha za Kumuwezesha Kurudi
Dsm alikosema ndio anafanya kazi ya TASAF.
Lakini
hadi jana anakamatwa akiwa kwenye jaribio la Kumtapeli Dreva wa
Mh:Makongoro Mahanga, ameshadanganya Madreva Wengi na bado amekuwa
akionekana Dodoma tofauti na maelezo yake kuwa anahitaji msaada wa
Nauli arejee Dsm tangu Bunge la Katiba Kuanza,Pia ameshukiwa kutapeli
watu wengi fedha likiwamo jaribio la Kuiba pikipiki eneo la Kituo cha
Polisi Dodoma.
Wakati
anakamatwa kulijitokeza watu mbalimbali waliopata kukutana naye na
kutapeliwa,Hivyo jeshi la Polisi limemkamata na kumpeleka kituoni kwa
hatua zaidi za Kisheria.
0 comments:
Post a Comment