WAMACHINGA WAPAMBANA NA POLISI KARIAKOO
Jeshi la
Polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwaondoa wafanyabiashara
ndogondogo (wamachinga) katika Soko Kuu la Kariakoo.
Hamisha
hamisha hiyo yenye baraka za uongozi wa mkoa zilianza mapema mwezi
uliopita kwa lengo la kuondoa biashara zisizo rasmi katikati ya jiji la
Dar es Salaam, pamoja na bodaboda, bidhaa zimwagwazo chini, mama ntilie
na vibanda vya vocha.
Majira ya
saa tisa alasiri magari ya polisi yaliwasili sokoni hapo huku yakiwa na
askari polisi na mgambo waliokuwa wamevaa fulana na kofia za Chama cha
Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (Talgwu), zenye rangi ya njano, na
kuanza kuwakamata wamachinga hao.
Askari
hao waliokuwa katika magari aina ya Land Rover Defender na Toyota
LandCruiser waliuvamia mitaa ya Kongo na Mchikichini kufanya oparesheni
hiyo kabla hawajalazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwaondoa
walengwa katika eneo hilo.
Hali hiyo
ilizua tafrani kwa wateja waliokuwa wakinunua bidhaa kwenye maduka hayo
walioenda kwa ajili ya kupata mahitaji yao walikimbia hovyo ili
kujiokoa kutokana na vurugu hizo.
Maduka
mengi ya mtaa huo, kuanzia kituo cha daladala hadi sokoni, yalilazimika
kufungwa kwa hofu ya kupoteza mali kutokana na vibaka wanaotumia nafasi
kama hizo kuiba vitu.
Kazi
haikuwa rahisi kwa askari hao kwani wamachinga kadhaa hawakuwa tayari
kuona wakikamatwa au kupoteza mali zao hivyo kulazimika kupambana kwa
kile kilichoonekana kama kuwa radhi ‘kufia mali’ zao. Wamachinga hao
waliokaidi amri halali ya jeshi hilo, walikamatwa na kuingizwa kwenye
gari la polisi .
Watu
walionekana wakikimbia hovyo na wengine wakipanda gari lolote bila
kujali linaelekea wapi ili mradi waondoke eneo la tukio kabla
hawajapatwa na lolote na kuumia au kuibiwa. “Sisi tutaenda wapi bwana.
Acha wafanye mambo yao wakiondoka tunarudi tena kuendelea na biashara
zetu,” alisema Hamis Jumanne, anayefanya biashara ya kuuza maji.
Kamanda
wa Polisi Mkoa kipolisi wa Ilala, Marietha Minangi alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kuwa zoezi la kuondoa wamachinga jijini ni endelevu
0 comments:
Post a Comment