Tuesday 10 June 2014

BOKO HARAM WATEKA WANAWAKE WENGINE 20 NCHINI NIGERIA



Wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Boko Haram wamewateka nyara wanawake 20 kutoka jamii inayohamahama Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
 
Wanawake hao walichukuliwa katika Makazi ya Gakini Fulani karibu na mji wa Chibok ambako zaidi ya wasichana wanafunzi 200 walitekwa nyara Aprili, mwaka huu.
Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa wapiganaji hao waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwalazimisha wanawake hao kuingia katika magari yao kabla ya kutoroka nao katika Jimbo la Borno.
 
Mlinzi mmoja wa kijiji alisema kuwa washambulizi hao pia waliwateka nyara wanaume watatu waliojaribu kuwazuia wasiondoke na wanawake hao. Hadi sasa jeshi halijasema lo lote kuhusiana na tukio hilo.
 
Katika  hatua  nyingine,  jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaua wapiganaji 50 katika kampeni yake dhidi ya magaidi mwishoni mwa wiki katika majimbo ya Borno na Aladawa.
 
Mfululizo wa mashambulizi Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo umeimarisha ukosoaji wa vyombo vya usalama vya Serikali.
 

Licha ya kuwepo kwa hali ya hatari katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wanajeshi hawajachukua hatua thabiti kukabiliana  na  hali  hiyo. 
Chanzo: BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA