Shabiki anayeonekana kama Ronaldinho alivamia mazoezi ya Argentina kwenye uwanja wa Belo Horizonte
Nyota akigoma kutoka: Messi akifurahia wakati shabiki akitolewa na maofisa, kufafana na Ronaldinho kulimfanya Messi acheke sana
MAZOEZI ya Argentina jana jumatano yalivamiwa na mtu moja mwenye sura inayofahamika duniani.
Wakati Lionel Messi na wachezaji wenzake wakijiandaa kuelekea mchezo wa ufunguzi wa kundi lao dhidi ya Bosnia siku ya jumapili, shabiki mmoja mwenye sura inayofanana na nyota wa zamani wa Brazil, Ronaldinho alivamia uwanjani.
Waargentina walimfurahia jamaa huyo lakini alitolewa na maofisa wa uwanja.
Umetukuka baba!: Shabiki akifuta kiatu cha kulia cha Lionel Messi baada ya kuvamia uwanjani wakati wa mazoezi
Mambo safi! Messi aliamua kumkumbatia jamaa.
Mashabiki wengi walivamia uwanjani na kumpigia magoti nahodha huyo wa Argentina, Lionel Messi huku wakifuta viatu vyake.
Messi alicheka tu na aliwakumbatia mashabiki hao na alimpa shabiki mmoja sweta lake kabla ya walinzi kumtoa.
Mashabiki wengine waliukimbilia mpira ambao Muargentina huyo alikuwa anautumia katika mazoezi.
Ajabu! mamia ya mashabiki wa Argentina walifurika uwanjani wakati timu yao ikijiandaa na mchezo wa ufunguzi wa kundi F dhidi ya Bosnia.
0 comments:
Post a Comment