Wednesday, 9 July 2014

TETESI ZA UASJILI KATIKA SOKA ,ULAYA


Uhamisho wa Luis Suarez kutoka Liverpool kwenda Barcelona bado unasuasua kutokana na kutokubaliana jinsi ya kukamilisha ada ya pauni milioni 75 (Daily Mail), beki wa kulia kutoka Ufaransa Mathieu Debuchy, 28, anatarajiwa kuwa na vipimo vya afya Arsenal, akijiandaa kuhama kutoka Newcastle kwa pauni milioni 7.9 (Guardian),
Newcastle huenda wakapewa Joel Campbell, 22, kama sehemu ya makubaliano ya Debuchy kwenda Arsenal (Newcastle Cronicle), Arsenal pia wanaweza kuwapa Newcastle beki wa kulia Carl Jenkinson, 22, katika makubaliano hayo (Daily Mail)
Barcelona wameungana na Manchester United kumsaka beki wa Borrusia Dortmund Mats Hummels, 25 (Daily Express), Liverpool wamelazimika kukubali kushindwa mbio za kumsajili mshambuliaji wa Barcelona, Alexis Sanchez, 25, ambaye anajiandaa kusajiliwa na Arsenal (Liverpool Echo), Samuel Eto'o anajiandaa kuungana na Ashley Cole kuichezea Roma, baada ya kuondoka Darajani (Daily Mail)
Liverpool wameambiwa lazima waongeze dau kufikia pauni milioni 25 iwapo wanataka kumsajili beki wa kati wa Southampton Dejan Lovren (Daily Star), Paris St-Germain wanajiandaa kutoa pauni milioni 47 kumnunua Angel Di Maria kutoka Real Madrid. Manchester United pia wanamtaka Di Maria, lakini huenda PSG wakawazidi kwa dau kubwa (Sky Sport Italia), Liverpool wanakaribia kukamilisha usajili wa Euro milioni 12 wa mshambuliaji wa Lille na Ubelgiji, Divock Origi. Origi anatarajiwa kwenda Liverpool kuzungumzia masuala binafsi (The Independent)
Real Madrid wamekamilisha uhamisho wa Toni Kroos, ingawa hautatangazwa rasmi hadi baada ya Kombe la Dunia. Kiungo huyo wa Bayern Munich amesaini mkataba wa miaka mitano kwa uhamisho wa pauni milioni 23 (Bild), Arsenal wanajiandaa kupanda dau kwa beki wa Ugiriki Kostas Manolas kuziba pengo la Thomas Vermaelen anayedhaniwa kuelekea Old Trafford.
Manolas atagharimu Euro milioni 10 (Daily Star), Manchester United huenda wakatumia mzozo uliozuka ndani ya bodi ya Valencia kwa kumnyatia kiungo kutoka Argentina Enzo Perez anayesakwa na Benfica (O Jogo). Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!(P.T)
Kutoka Kwa Salim Kikeke

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA