Wednesday 16 July 2014

UKATILI:JINSI KAMPUNI YA UWINDAJI ILIYOFUTIWA LESENI YAKE, GMS ILIVYOKUWA IKIFANYA KAZI ZAKE KINYUME NA MAKUBALIANO!



Kampuni ya uwindaji ya Gree Miles Safari Limited(GMS) iliyokuwa ikifanya kazi zake za uwindaji Tanzania ilifutiwa leseni yake rasmi wiki iliyopita kutokana na kampuni hiyo kwenda kinyume na makubaliano na sheria za uwindaji za Tanzania.
Ilifika wakati ambapo kampuni hiyo ilithubutu  kuwinda hadi ndege wakati ilikuwa hajaruhusiwa ama kukubaliana na serekali ya Tanzania kufanya hivyo.

Vibaya zaidi kampuni hiyo ilianza hata kukamata wanyama wadogo na kuwachukua wakati hilo pia halikuwa ndani ya makubaliano yake na serekali.

Hata hivyo, baada ya waziri Nyalandu kuifutia leseni, kampuni hiyo iliruhusiwa kufungua mashtaka mahakamani kutokana na hasara ambayo itakuwa imesababishiwa ili sheria ichukue mkondo wake kama itaona kuwa imeonewa kwa kitendo hicho.


Angalia picha zake hapo chini ili upate kuona shughuli za kampuni hiyo kwa ujumla pamoja uvunjifu wa sheria na makubaliano yake na serekali ya Tanzania:



Kampuni hiyo ikiwinda ndege


kampuni ya GMS ikiwa imekamata ndege


Ikiwa imemkamata mnyama mdogo kwa lengo la kumbeba


Ikiwa imemkamata mnyama kwa lengo la kuondoka naye




Wawindaji wa GMS wakiwa wamemkamata ndege


Hapa wawindaji wa GMS wanampakia mnyama waliokwisha kumuua kwenye gari


Mnyama aliyejeruhiliwa kwa risasi. Anamaliziwa kwa risasi nyingine hapa chini:




 aliyekwisha kuuawa kwa risasi, tayari kuchukuliwa


Wawindaji wakiwa mawindoni


Wawindaki wakimpakia nyama waliyemuua


Mnyama aliyeuawa, tayari kwa kusafirishwa


Sasa swali langu ni je, mpaka muda huu serekali inaposhtuka kuwa wawindaji hawa wanavunja sheria ni kwa kiasi gani Tanzania imepata hasara kubwa?

Na je, ina maana kuwa watanzania wameshindwa hata kuwa na makampuni ya uwindaji mpaka kuyasajili makampuni ya wageni ambao hawana  uchungu na taifa letu?

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA