#BAD_NEWS GEEZ MABOVU AFARIKI DUNIA,IRINGA
Msanii Geez Mabovu kutoka Iringa Amefariki Dunia usiku huu mida ya saa moja akiwa huko Iringa na hii ni baada ya kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Malaria.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Iringa, Geez amefariki jioni hii. Alienda kwao wiki moja na nusu iliyopita ambako alianza kuugua mfululizo. Taarifa zaidi zinakuja.
December 27 mwaka jana, hitmaker huyo wa Mtoto wa Kiume alizidiwa ghafla kabla ya show iliyokuwa ifanyike mjini Iringa kwenye ukumbi wa Twista Night Club alikokuwa atumbuiza na rappers wengine wakiwemo Wakazi, Songa, Jan B na Chidi Benz.
Tutakukumbuka kwa mengi sana kaka yetu, ikiwa ni pamoja na kazi zako nzuri za sanaa ya muziki.
R.I.P #GeezMabovu , Mungu Amekupenda Zaidi.