22:19 |
story na Kd Mula
Mashabibiki wa klabu ya soka ya Liverpool inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza wamepata ahueni mara baada ya mshambuliaji wa timu hiyo Daniel Sturidge kurejea mazoezini baada ya kuwa majeruhi kwa zaidi ya miezi miwili.
Akithibitisha kurejea kwake rasmi mazoezini kupitia mtandao wa twitter Sturigde ameandika kuwa amefurahishwa na kupona kwake na kutoa shukrani zake kwa Mungu.
Ikumbukwe Sturidge aliichezea Liverpool kwa mara ya mwisho katika mechi dhidi ya Totenham na kuisaidia kupata ushindi wa goli tatu.
Sturidge anarejea wakati muafaka kwani Liverpool imekuwa ikiyumba na hasa kuonesha ubutu mkubwa katika safu ya ushambuliaji kwani Mario Balletili bado hajafanikiwa kuifungia Liverpool goli katika ligi kuu licha ya kucheza mechi zaidi ya nane.