HUYU NDIYE RAIA WA MAREKANI ALIYECHINJWA NA KUNDI LA IS
Kanda
moja ya video iliowekwa mtandaoni inaonyesha mauaji ya mtu wa kutoa
huduma za misaada raia wa Marekani Abdul Rahman Kassig ambaye alikuwa
anajulikana kama Peter Kassig kabla ya kutekwa nyara na wanamgambo wa
Islamic State nchini Syria mwaka uliopitaVideo hiyo inamuonyesha
mwanaume mmoja anayeonekana kuwa mwanachama wa Islamic State akiwa na
kisu mkononi na maandishi yanayosema kuwa Peter Kassig ameuawa.
Bwana Kassig ambaye anajulikana kama Peter alitekwa nyara mwaka uliopita.Mnamo mwezi Octoba kanda nyengine ya video ya kifo cha mfanyikazi mwengine wa misaada kutoka Uingereza Alan Henning iliisha huku Kassig akitishiwa.
-BBC
Peter Kassig mda mchache kabla ya kukatwa shingo na wapiganaji wa IS
Kanda
hiyo pia ina picha za watu kadha waliouawa ambao wanasemekana kuwa
wanajeshi wa Syria waliokuwa wametekwa nyara.Marekani imesema kuwa
inafanya juhudi za kubaini chimbuko la kanda hiyo.Bwana Kassig ambaye anajulikana kama Peter alitekwa nyara mwaka uliopita.Mnamo mwezi Octoba kanda nyengine ya video ya kifo cha mfanyikazi mwengine wa misaada kutoka Uingereza Alan Henning iliisha huku Kassig akitishiwa.
-BBC