WANAHABARI WALIMINYA SAUTI ZA WANAWAKE UCHAGUZI MKUU – UTAFITI
Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga akifungua warsha ya wadau wa vyombo vya
habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu
wenyeulemavu, ambayo pia ilishirikisha wahariri kutoka vyombo anuai vya
habari nchini Tanzania. Warsha hiyo iliandaliwa na TAMWA.
Mwezeshaji
katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya
wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, Valeria Msoka
akizungumza katika warsha hiyo.
Mwezeshaji
katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya
wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, Valeria Msoka (kulia)
akizungumza katika warsha hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga (kulia) akifungua warsha ya wadau wa
vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu
wenyeulemavu, ambayo pia ilishirikisha wahariri kutoka vyombo anuai vya
habari nchini Tanzania. Warsha hiyo iliandaliwa na TAMWA.(P.T)
Bi.
Stella Jairos ambaye ni miongoni mwa wagombea walioshiriki Uchaguzi Mkuu
2015 wakizungumza kuelezea changamoto anuai katika warsha hiyo. Bi.
Jairos aligombea Ubunge Vitimaalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Mkoa wa Dodoma.
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimesema wanawake
waliogombea nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 walikosa nafasi
ya kutosha kuzungumza kwenye vyombo vya habari. Alisema utafiti mdogo
walioufanya katika vyombo vya habari kadhaa ulibaini kuwa ni asilimia 11
tu ya wanawake wagombea ndio walipata nafasi ya kuandikwa katika
magazeti wakati wa uchaguzi huo.
Takwimu
hizo zilitolewa jana katika semina ya wadau wa vyombo vya habari pamoja
na baadhi ya wagombea na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga
alipokuwa akifungua semina hiyo ambayo pia ilishirikisha wahariri kutoka
vyombo anuai vya habari nchini Tanzania.
Alisema
katika utafiti huo uliofanywa kwa miezi miwili yaani Septemba na Oktoba
2016 kwenye magazeti sita ulibaini kati ya vyanzo vya habari 2577
vilivyotumika kwenye habari za Uchaguzi Mkuu, wanaume waliotumika kama
vyanzo walikuwa 2256 ikiwa ni sawa na asilimia 88 huku wanawake 303 kama
vyanzo hii ikiwa ni asilimia 11 tu.
Mkurugenzi
huyo Mtendaji wa TAMWA alisema utafiti pia uliainisha kuwa wanaume
waliongoza katika makundi yote ya mada za habari hata zile ambazo
hazikuwa zikihusiana na uchaguzi huo. Aliongeza kuwa katika utafiti huo
ilikuwa ni nadra sana kupata habari ambazo zipo katika kurasa za mbele
huku vyanzo vyake vikiwa vimetokana na wanawake. Habari za wanawake
zilianza kujitokeza kuanzia kurasa za nne na kuendelea.
“…Kwa
mujibu wa matokeo ya ufuatiliaji wa habari za magazeti, wanawake kwa
ujumla waliogombea na wasiogombea kote nchini walikabiliwa na
unyanyasaji kama vile kufanyiwa ghasia, na vitisho wakati wa kampeni na
siku ya uchaguzi. Pia wanaume walificha kadi za kupigia kura za wanawake
zao, wanaume waliwalazimisha wake zao kuwapigia kura wagombea ambao
wanawataka hata kama mwanamke hamtaki, utumiaji wa lugha ya matusi dhidi
ya wagombea wanawake na wakati wa kampeni kuna baadhi ya wagombea
wanawake walikamatwa na kutishiwa kwa tuhuma za kutotii amri ya Jeshi la
Polisi,” alisema Sanga katika taarifa yake akifungua semina hiyo.
Baadhi ya
wagombea walioshiriki katika uchaguzi Mkuu 2015 wakizungumza kuelezea
changamoto anuai katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa
habari pamoja na wagombea hao.
Wanahabari waliminya sauti za wanawake Uchaguzi Mkuu – Utafiti
Baadhi ya
wagombea walioshiriki katika uchaguzi Mkuu 2015 wakizungumza kuelezea
changamoto anuai katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa
habari pamoja na wagombea hao.
Baadhi ya
washiriki katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa
habari pamoja na baadhi ya wagombea walioshiriki katika Uchaguzi Mkuu
2015 kuzungumzia changamoto za kutopewa nafasi wagombea wanawake, vijana
na walemavu kwenye vyombo vya habari.
Kwa
upande wao wanawake waliogombea wakizungumza katika semina hiyo walisema
vyombo vya habari kiujumla havikutoa nafasi sawa kwa wagombea hasa
wanawake na vingi vilikimbilia kutoa habari za wagombea wenye majina na
maarufu kwa wanajamii. Bi. Stella Jairos ambaye aligombea Ubunge
Vitimaalum Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dodoma alisema wanawake walemavu
mbali na kukosa fursa kwenye vyombo vya habari walikabiliwa na
changamoto mbalimbali zilizofifisha mafanikio katika kinyang’anyiro cha
uchaguzi huo.
Naye
Loyce Kibona aliyegombea upande wa vyama vya upinzani katika uchaguzi
huo alisema licha ya vyombo vya habari kuwa ni changamoto kwao kupata
nafasi ya kusikika bado hali ya kujiamini kwa wanawake na kukatishana
tamaa kunaendelewa kukwamisha mafanikio ya kundi hilo hivyo kuwataka
wanawake kuungana mkono.
Imeandaliwa: www.thehabari.com
Imeandaliwa: www.thehabari.com
0 comments:
Post a Comment