SERIKALI YAFUNGUKA KUHUSU MAUAJI YA KITETO
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb)
akizungumza na Kamati ya Uongozi ya Bunge jana na kuainisha hatua
madhubuti za kuchukuliwa na serikali ili kukomesha mauaji baina ya
wakulima na wafugaji yanayoendelea Mkoani Manyara wilaya Kiteto na
sehemu nyingine nchini.
Wajumba
wa Kamati ya Uongozi ya Bunge wakimsikiliza Waziri Mkuu kwa umakini
mkubwa alipokuwa akitanabaisha jinsi Serikali isivyopendezwa na mauaji
ya Kiteto na jinsi ilivyojipanga kukomesha kabisa mauji hayo.
Naibu
Spika na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb)
akiwashukuru wajumbe wa Kamati ya Uongozi kwa jinsi walivyozungumza na
Mhe, Waziri Mkuu kwa moyo wa kizalendo kwa nchi yao.
Katibu
wa Bunge Dkt Thomas Kashililah (kushoto) akitoa ushauri kwenye Kamati
ya Uongozi jinsi ya kuwasilishwa Bungeni taarifa za Tume mbalimbali jana.
Picha na Prosper Minja-Bunge