MKUU WA WILAYA AAGIZA WANAFUNZI 24 WALIOPATA MIMBA WARIPOTI POLISI
09:30 |
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani,Nurdin Babu ameagiza wanafunzi24 wa Sekondari mbalimbali Wilayani humo waliopata ujauzito kuripoti kituo cha polisi November25 mwaka huu ili wasaidie kutoa ushirikiano wa kuwakamata wahusika waliowapa mimba na kuweze kukamatwa.
Sambamba na wanafunzi hao pia wazazi au walezi wa wanafunzi hao wametakiwa kuripoti wakiwa na watoto wao ambapo atazungumza na wazazi pamoja na wanafunzi hao ili kujua tatizo ni nini.
Babu alisema taarifa za watoto 26 walipata ujauzito katika kipindi cha Januari hadi Oktoba si nzuri na lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe ili kuondokana na matatizo hayo ndani ya jamii.
Alisema idadi ya wanafunzi waliokatishiwa masomo ni kubwa na Serikali haiwezi kulifumbia macho suala hilo.
-EDDYBLOG