CHEKI SHEREHE MIAKA 53 YA UHURU WA TANZANIA BARA ZILIVYOFANA DAR ES SALAAM
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara CCM, Philip Mangula. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, akisalimiana na waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.Baadhi ya viongozi wa nchi wakiwa jukwaa kuu. Askari wa majeshi ya ulinzi na usalama wakitoa heshima kwa Rais Kikwete. Haya ni maonyesho ya halaiki. Baadhi ya wananchi waliofika kwenye sherehe hizo.
RAIS Kikwete leo ameongoza sherehe za kuadhimisha miaka 53 tangu Tanzania Bara ipate uhuru wake Desemba 9 1961. Hafla hiyo ilifanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali nchini na wawakilishi wa nchi za nje walioshuhudia burudani ya kwaya, gwaride, halaiki, ngoma za asili, sarakasi na michezo mingineyo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
0 comments:
Post a Comment