Saturday 3 January 2015

WANANCHI KINONDONI WASHITUSHWA NA UBOVU WA DARAJA LA KIBWEGERE SHULENI



Hili ndio daraja la Kibwegere njia ya shuleni ambalo limezua maswali kwa wananchi
Story na Kd Mula 
Wananchi wa wilaya ya Kinondondi eneo la Kibamba Kibwegere wameshitushwa na ubovu wa daraja ambalo limeanza  limebomoka na kutuama kwa maji hata kabla ya kukabidhiwa kwa Serikali.

Wakizingumza na mwandishi wetu wananchi hao kwa sharti la kutopigwa picha walimshutumu mkandarasi wa ujenzi huo wakisema limejengwa chini ya kiwango.
Sehemu ya daraja hilo iliyobomoka

"Hebu angalia, hili daraja halina  muda tangu ujenzi wake umekamilika lakini cha kushangaza hata kabla halijakabidhiwa tayari limebomoka,jamani fedha za serikali zimetupwa" alisema mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Mariamu.


Daraja hili lililopo njia ya Kibwegere shuleni ni kiunganisho muhimu kwa wakazi wanaoishi Kibwegere hasa kulekea shule za msingi na sekondari za Kibwegere.


Akizungumza na mwandishi Salim Juma alisema,"Hizi ni mvua za pili tangu mkandarasi amemaliza kazi yake lakini tazama namna palivyobomoka na maji yalivyotuama,kweli utasema mkandarasi amefuata vipimo sahihi? kama hivi ndivyo miradi ya maendeleo invyotekelezwa basi tuna safari ndefu.

Mwandishi wetu alijionea sehemu ya daraja ambapo maji yametuama na kuleta adha kwa watumiaji wa daraja hilo.

Namna maji yaliyotuama yakileta adha kwa watumiaji wa daraja hilo.

Funguka Live ilitafuta uwezekano wa kumpata diwani wa eneo hilo Ndugu Issa Mtemvu ambapo hakupatikana mara moja kutokana na majukumu.


Hii si mara ya kwanza kwa miundombinu kujengwa chini ya kiwango hapa nchini Tanzania, Wito kwa Serikali ni kusimamia miradi hii na kuweka masharti magumu kwa atakaebainika kufanya kazi chini ya kiwango kwani usalama wa raia wanaotumia miundo mbinu hii huwa hatarini.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA