Elimu: Ebola inatufundisha na kutukumbusha ustarabu na kanuni za kiafya
Zikiwa ni siku kadha zimepita tangu ugojwa huu kugundulika tena lakini bado dawa ya kutibu ugonjwa huu haijapatikana kama ilivyo Ukimwi.Kwa magonjwa ya namna hii kimbilio huwa ni kujikinga ,kutambua kanuni za kujikinga, kuwa na taarifa sahihi kwa wakati sahihi na kufanya maamuzi sahihi.
Hilo ndilo la jambo la msingi kwa sasa na kila familia inatakiwa kulizungumza jambo hili kwa kina huku taarifa sahihi zikitumika zaidi.Hii ni nafasi nzuri kwani itasaidia kujikinga mapema kabla ugonjwa huu haujafika katika ngazi za familia na nchi.
Wakati wote tumekuwa tukishauriwa na wataalamu wa Afya kunawa mikono kwa kufuata kanuni lakini wangapi wanafanya hivyo na wangapi wanasimamia hilo katika ngazi za familia bado ni changamoto lakini bado watalamu wanaendelea kushauri na kusisitiza kuwa kufuata kananu za unawaji mikono ni namna nzuri ya kujikinga na magonjwa hasa nykati hizi ambzo Ebola imekuwa tishio kwa dunia nzima.Huu ni wakati ambao katika kila ngazi ya familia lazima kanuni hizi za unawaji mikono zifuatwe kwa mfano na sio maneno.
Katika ngazi za familia wazazi hujadili kuhusu maadili zaidi hasa ya mavazi na adabu lakini hizi ni nyakati za kuanzisha mtindo mpya wa kuwa siliana kwa kina kuhusu Ebola .Wengi mtakuwa mashahidi jinsi ilivyo kuwa changamoto kujadili kuhusu Ukimwi na hata maswala ya kiafya katika ngazi za famila.Nyakati hizo zimepitwa tusije kufanya makosa tena ni jukumu la familia kuwa na taarifa sahihi kuhu Ebola na maswala mengine ya kiafya maana hali si nzuri kwa wenzetu ndio maana wasahili wakasema ukiona mwenzio ananyolewa basi wewe tia maji.
Ukiwa mjini hata vijini watu hupenda kusalimiana kwa kupeana mikono ila wakati huu lazima tujifunze usatarabu mpya na kanuni za kiafya ili kujikinga na Ebola huu ni wakati wa kufuata usatarabu na kuzingatia kanuni za afya.
Tusikubali kuwa na utamaduni wa kujua wangapi wamekufa au wangapi wame ambukizwa tuu hii pekee yake haitoshi tubadili mtazamo wangapi wamejikinga na kubadili mwenendo ili na sisi tuweze kujifunza kanuni ili tujikinge.
Tusikubali kujua neno Ebola pekee yake wakati nafasi na fursa ya kujifunza kupitia mitandao ni pana.Vijana na jamii ni lazima kuzinduka ili tutafute taarifa kuhusu Ebola ili tuweze kufanya uamuzi sahihi na kujikinga.
Ni ugwana kutumia vifushi ulicho jiunga hii leo kutafuta taarifa sahihi kuhusu Ebola na kujenga mazoea ya kujua usatarbu na kanuni za kiafya maana waswahili husema bora kinga kuliko tiba.
Taarifa inayo patikana katika tovuti ya Al-Jazeera zinaonyesha kuwa asiliia 70 ya watu wanaoambukizwa Ebola hufaliki [1] huku gazeti la Daily news lenye kichwa cha habari (Ebola orphans in west Africa face stigma) likiwa na taarifa linaonyesha njinsi gani ugonjwa huu unazidi kuathiri maisha ya familia katika bara la Afrika na watoto wakibaki yatima.
Hatuna namna zaidi ya kubadili ustarabu na kufuata kanuni za kiafya ili kujikomboa.Katika ngazi za familia lazima jukumu hili la kujikinga na kuzungumza kuhusu afya liwe endelevu na kwa mifano.
[1] http://www.aljazeera.com/indepth/interactive/2014/08/infographic-deadly-ebola-epidemic-west-africa-20148248162913356.html
Imeandaliwa na
Kiduo Mgunga, Mwanafunzi wa Mawasiliano ya Jamii katika chuo cha SMMUCo, Mwaka wa tatu
.
.
0 comments:
Post a Comment