Tuesday 24 March 2015

AMFUMANIA DADA NA MUME WAKE WAKIFANYA MAPENZI:;NA KUWANYANG'ANYA NGUO



Mwanamke aliyejulikana kwa jina Ting Su nchini China amemwacha mumewe na dadake bila nguo barabarani baada ya kuwakuta wakifanya mapenzi.
Ting Ting Su aligundua kwamba mumewe alikuwa akimsaliti na dadaake ndipo alipoamua kuwafuata hadi katika kituo kimoja cha maduka akitumia teknolojia katika simu yake ambapo aliwapata wakichemshana katika gari la mumewe.
 Wawili hao walitoka ndani ya gari hilo bila nguo kwa kubabaika ili kujaribu kumuelezea kilichokuwa kikiendelea lakini waliachwa na mshangao mkubwa wakati Ting alipoingia ndani ya gari hilo na kuondoka kwa haraka na kuwaacha wawili hao barabarani bila nguo.
 Kwa mujibu wa gazeti la Metro,shahidi aliyejulikana kama You Meng alisema walioshuhudia kisa hicho walibeba simu zao na kuanza kuchukua picha na yeye hakubakia nyuma.
Mumewe aligonga dirisha la gari hilo na kumpigia kelele mkewe lakini hakujali kamwe aliliondosha gari hilo kwa haraka.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA