IS YARIDHIA KUUNDA USHIRIKIANO NA KUNDI LA BOKO HARAM LA NIGERIA
Kundi la Dola ya Kiislam (IS) limekubali wito wa kundi laNigeria la Boko Haram kutaka uhusiano na kukubali kuwatii IS.
Katika sauti iliyorekodiwa msemaji wa IS amenukuliwa akisema kuwa lengo la kutanua utawala wa dola ya Kiislam limeongezeka na kufika Afrika ya Magharibi.
Wiki iliyopita Boko Haram walituma kwa njia ya mtandao ujumbe unaotaka kuwepo ushirikianoa na kundi la IS.
Boko Haram walianza harakati za kutaka kushinikiza uwepo wa utawala wa Kiislana kaskazini mwa Nigeria tangu mwaka 2009.
0 comments:
Post a Comment