WAUGUZI WAINGIA KWENYE KASHFA ARUSHA, NI BAADA YA KUWAPIGA NA KUWADHALILISHA WAGONJWA
07:38 | No Comments |
Picha toka maktaba |
wakizungumza katika kikao cha wadau wa afya wa mkoa wa Arusa baadhi ya wananchi waliathiriwa na tatizo hilo wamesema tatizo ni kubwa zaidi katika maeneo ya pembezoni ambapo asilimia kubwa ya wanawake wanatoka katika familia maskini zisizo na uwezo hasa za jamii ya wafugaji.
Baadhi ya watendaji akiwemo mkuu wa wilaya ya Monduli Bw,Jowika Kasunga mkuu wa wilaya ya arusha Christopher Kangoye nanaibu meeya wa jiji la Arusha Prosper Msofe wamesema hatuailiyofikia sasa haivumiliki na licha ya kumtupia lawama mganga mkuu wa mkoa wameiomba jamii kuendelea kutoa ushirikiano wa kuwabaini watendaji.
Akizungumzia tatizo hilo mganga mkuu wa mkoa wa arusha Dr.Frida Mokiti amesema tatizo hilo lipo na lina athari kubwa na kwamba licha yakuchukua hatua aadhi ya mambo yako nje ya uwezo wao.
Malalamiko ya wagonjwa juu ya wakiwemo akina mama wajawazito yakudhalilishwa na baadhiya watendaji wa sekta ya afya kwa muda mrefu sasa yamekuwa yakiendelea kusikika katika kona mbalimbali nchini jambolinaloonyesha kuwa ngazi zinazohusika hazijachukua hatua stahiki za kukomesha tatizo hilo.
0 comments:
Post a Comment