Saturday 28 March 2015

MR & Miss Talent Mwenge Catholic University ILIKUWA BOMBA SANA:CHEKI MWENYEWE

 Mr & Miss Talent Mwenge Catholic University Mkude Robert Mwisaria na Noela Bernard Masao 


Kwa mara ya tatu mfululizo tangu 2012 shindano la kumsaka MR & Miss Talent Mwenge Catholic University lilifana sana usiku wa kuamkia jumamosi katika viwanja vya Kili Home Bar & Restaurant mkoani Kilimanjaro na kufanikiwa kuwapata wale wanaolishikilia taji hilo hadi pale mwaka 2016.


Shindano hilo ambalo lilijumuisha wadau mbali mbali toka viunga vyote vya kanda ya kaskazini lilikuwa chini ya udhamini wa Serengeti breweries kwa hisani ya kinywaji cha SMIRNOFF,Akiba Comercial Bank,Mwenge Catholic University,Innosykes Computers,Image Transfers, Msafiri  Maua Medics pamoja na  Kili Home Bar & Restaurant lilianza kupata uhai majira saa mbili usiku hadi pale washindi walipopatikana.
Washiriki wa kike waMr & Miss Talent Mwenge Catholic University wakicheza mbele ya waliohudhuria
 Washiriki wa kiume waMr & Miss Talent Mwenge Catholic University wakicheza mbele ya waliohudhuria
Katika kuhakikisha MR & Miss Talent anakuwa na vigezo vyote, washiriki wapatao kumi na moja ambao ni wanafunzi wa Mwenge Catholic University wakiwemo wasichana wanne na wavulana sita walitakiwa kuonesha  mitindo mbali mbali ya mavazi ikiwemo vazi la kawaida (casual wear) ,vazi la ofisini, vazi la usiku, ubunifu pamoja na vipaji vyao.
Wawakilishi wa  uongozi wa  Mwenge Catholic University wakiwa makini kushuhudia burudani iliyokuwa inaendelea


Noela Bernard akiwa katika kuonesha vazi la kawaida


kila mshirirki aliweza kuonesha kipaji chake


Mshiriki Happy Munuo akionehsa kipaji chake cha ubunifu

Majaji wakiwa makini kutizama nini washiriki wanafanya
Chini ya usimamizi mzuri wa Chief jaji Lui Ndakideme akisaidiana na majaji Furaha Hamadi, Uenice Mmari pamoja na Mr Benson washiriki walipata mchujo wa awali na kwa wale alioingia tano bora walikuwa ni Samuel Sixbert,Mkude Robert,Raphael Nyandi Suzan Modest,Happy Munuo pamoja na Noela Bernard Masao ambapo waliulizwa maswali na majaji na baada ya hapo MR & Miss Talent wakatangazwa ambao ni Mkude Robert Mwisaria na Noela Bernard Masao.
Wawakilishi wa Akiba Comercial Bank nao walikuwa makini kufuatila kila tukio

Chief jaji Lui Ndakideme akiwatangaza washindi
Mkude Robert Mwisaria akimshukuru Mungu mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi
 Mr & Miss Talent Mwenge Catholic University Mkude Robert Mwisaria na Noela Bernard Masao 

Kama ilivyoada burudani ni sehemu muhimu ya shughuli kama hizi wasanii kadha wakadha toka mkoani Kilimanjaro walipanda kwa steji na kuwatumbuiza mamia ya wadau waliohudhuria kivutio kikubwa kikiwa ni "Diamond wa Moshi" ambaye alokonga nyoyo za waliohudhuria halfa hiyo.
Mkude Robert Mwisaria akiwa na designer wake Andrew kalema mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi,
Diamond wa Moshi akifanya yake stejini 
Burudani ya sarakasi nayo ilikuwa sehemu ya tukio

warembo hawa nao waliwakilisha vyema



  2 comments:

  1. Najivunia kuongoza shoo nzima kwa ushirikiano na wazira ya social mwenge catholic university lakin zaidi najivunia kuwa disigner WA washindi watatu WA kiume watatu,WA pili na wavkwanza bwana mkude Robert alisitahili kushinda nilianza kumuandaa zamani na kwa jitihada za hali ya juu

    ReplyDelete

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA