ZITTO KABWE ACHAGULIWA KUIONGOZA ACT-WAZALENDO:CHEKI PICHA
Mwanasiasa kijana, Zitto Kabwe, amechaguliwa kuwa kiongozi wa chama kipya cha siasa cha upinzani ACT Wazalendo, katika uchaguzi uliokamilika usiku wa kuamkia leo Jumapili Machi 29, 2015.Kwa mara ya kwanza chama hicho ambacho katika katiba yake, kinaonyesha patakuwa na viongozi wakuu, wakiongozwa na kiongozi wa chama, mwenyekiti wa chama, makamu wenyeviti wawili kutoka bara na visiwani, katibu mkuu, na manaibu katibu wakuu wawili kutoka pande zote za muungano kitakuwa chini ya uenyekiti wa mwana mama Mwanasheria msomi.
Matokeo hayo yanaonyesha, mwanamama huyo, Anna Mghwirim, ndiye aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, makamu mwenyekiti bara, Shaban Mambo, na makamu mwenyekiti Zanzibar, Ramadhan Suleiman Ramadhan.
Katibu Mkuu na manaibu wake, wanasubiri mapendekezo ya kamati Kuu ya chama ambayo ilitarajiwa kukamilisha kazi yake mapema alfajiri ya Jumapili. Pichani kiongozi huyo wa chama, Zitto Kabwe, akilakiwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho, wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika kwenye ukumbi wa Kadinali Rugambwa, Oysterbay jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 28, 2015. Zitto alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama hicho nafasi ambayo kwa katiba ya chama hicho ndiyo ya juu zaidi. Chama hicho kitazinduliwa rasmi Jumapili Machi 29, 2015 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
Zitto akionyesha alama ya chama ambayo ni "Uwazi"
Zitto akihutubia wajumbe
Zitto akihutubia wajumbe wakati wa uchaguzi huo
Zitto akipongezwa
Wajumbe wakiserebuka, wakati wa uchaguzi huo
Wajumbe wakifurahi kwa kushikana mikono kuonyesha umoja
Wajumbe wakipiga kura
Askofu Gerald Mpango akiongoza sala
Mzee Kastiko, akiwakilisha waislamu kuomba dua
Aliyekuwa katibu mkuu wa muda wa ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba, akihutubia
Msimamizi wa uchaguzi huo, Profesa Kitila Mkumbo
0 comments:
Post a Comment