Monday 2 March 2015

Mwili wa Kapteni Komba kuagwa leoo karemjee jijini Dar

Mwili wa aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi na Mkurugenzi wa kundi la uhamasishaji chama cha CCM LA Tanzania One Theatre (TOT), Kapteni Mstaafu John Komba unatarajiwa kuagwa leo katika viwanja vya Karimjee.

Mwili huo utaagwa kuanzia saa nne asubuhi kabla ya kusafirishwa kwenda Mbinga kwa maziko siku ya Jumanne.
  
Kifo cha Marehemu Komba kinakuwa ni pigo jingine kubwa katika tasnia ya Burudani kutokana na mchango wake, na kwa niaba ya wadau wengine wa tasnia hiyo, blog hii  iliongea na Asha Baraka kutoka msibani, ambaye alieleza kuwa Kapteni Komba ni mfano wa kuigwa na wasanii Wengine kutokana na kujituma kwake katika sanaa, akiwa pia na mchango mkubwa katika kukitangaza chama cha mapinduzi kupitia sanaa yake hiyo.
  
Marehemu Kapteni Mstaafu John Komba alifariki dunia juzi kwa tatizo la shinikizo la damu katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahala pema peponi Amina.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA