Monday 23 March 2015

SHINDANO LA KUMSAKA DJ MKALI KANDA YA KASKAZINI LAFANA :CHEKI HAPA

Ikiwa ni kwa mara ya kwanza kampuni ya Viceroy kuandaa mashindano ya kumtafuta dj bomba mwenye ujuzi mkubwa kwa ukanda wa kaskazini hatimaye mshindi apatikana.
 CLUB D
Mashindano haya yalifanyika jana jijini Arusha maeneo ya Club D ambapo judge mkuu wa mashindano hayo alikuwa ni dj PQ kutoka clouds fm,clouds radio zilizopo jijini Dar es Salaam.
BAADHI YA WASHIRIKI
Mashindano haya ambayo yalisimamiwa na kampuni ya vinywaji vikali TDL(Tanzania Distillers Limited) kupitia kinywaji chake cha Viceroy ambapo kupitia promotion zao waliweza kutangaza mashindano hayo kupitia mikoa mitatu Manyara,Arusha pamoja na Kilimanjaro.
Baada ya kutoa fursa hiyo vijana wengi katika mikoa hiyo mitatu waliweza kuchukuwa fomu zao za usaili kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo ambayo fainali zake zilifanyikia katika jiji la Arusha ndani ya club ya kisasa Afrika Mashariki iitwayo Club D.
DJ VIRUS AKIWA CLUB D KWA NJE KABLA YA MASHINDANDO
Mpaka mwisho wa tarehe ya kuchukua fomu tayari washiriki 15 waliweza kupatikana na hatimaye kampuni hiyo iliweza kuandaa mchujo wa kwanza ambao waliweza kuwapata washiriki 8,siku iliyofuata mchujo mwingine uliweza kufanyika ambapo walipatikana ma Dj watano bomba Dj Virus(Moshi), Dj Kito(Moshi), Dj Bray(Arusha), Dj Q(Arusha), pamoja na Dj Ally(Arusha).
“Kiukweli nimefurahishwa sana na mchuano huu lakini nimeweza kuona changamoto nyingi sana kutoka kwa washiriki wetu moja ya changamoto ni mashine
ambayo walikuwa wanatumia washiriki, hii mashine ni kubwa sana(Pionner CDJ 800) hivyo ilikuwa ngumu sana kwa baadhi ya washiriki kuitumia”alisema Mr Mrema ambaye ni zone Manager wa kampuni hiyo.
Kabla ya fainal hizo kufanyika washiriki wote watano waliweza kupata nafasi ya kutembelea kituo cha redio kilichopo jijini Arusha kijulikanacho kama Radio 5 kuzungumzia juu ya fainali hizo ambapo kila dj aliweza kuzungumza kwa mtazamo wake mwishoni wa mazungumzo kila dj aliweza kupewa nafasi ya kuonyesha ujuzi wake katika mashine.
Hatimaye siku ya jumamos fainali hizi ziliweza kufanyia pale club D Arusha ambapo mchuano ulianza,Mzunguko wa kwanza ilianza kwa kila dj kupewa dakika tano za kuonyesha ujuzi wake  mpaka mwisho waliweza kupatikana ma dj wanne Dj Virus(Moshi), Dj Kito(Moshi), Dj Bray(Arusha), pamoja na Dj Ally(Arusha).
Baaa ya kuwapata ma dj hao mzunguko wa pili ulianza kwa kila dj kupewa dakika 3 za kuonyesha ujuzi wake tena na hatimaye hapo ndipo mshindi alipoweza kupatikana, mshindi wa kwanza alitokea jijini Arusha Dj Bray, mshindi wa pili alitokea Moshi Dj Virus na mshindi wa tatu alitokea Arusha, ushindi ambao ulitangazwa na Dj PQ.
Mshindi wa kwanza Dj Bray aliweza kuzawadiwa mashine aina ya Pionner CDJ 900 yenye thamani ya shillingi million 8, mshindi wa pili Dj Virus alipewa headphone aina ya beats by dre yenye thamani ya shillingi laki 4, saa,t-shirt-chupa ya Viceroy ya ml 750 pamoja na kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusomea u dj katika chuo cha Dj PQ kwa muda wa miez mitatu bure na mshindi wa tatu Dj Ally aliweza kupewa saa,t-shirt na chupa ya Viceroy ya ml 750.
Dhumuni hasa la mashindano haya ni kuwafanya wale ma dj wote chipukizi waliopo katika tathnia hii ya burudani ya muziki kuweza kuonekana na jamii kuwa wao pia wanauwezo pamoja na kuwafanya waweze kupata ajira sehem tofauti tofauti.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA