YAJUE MATUNDA AINA 5 YANAYOWEZA KUKUPATIA MUONEKANO MZURI WA NGOZI YA MWILI WAKO
Baadhi ya watu wamekuwa wanachukulia kirahisi ulaji wa matunda, lakini unapaswa kujua kwamba matunda ni muhimu kwa afya zetu kwani yanatukinga na magonjwa mbali mbali na pia hutengeneza muonekano mzuri wa ngozi ya miili yetu.
Kunakila
sababu za kukubali kuwa matunda ni muhimu sana kwa afya zetu kwa sababu
huongeza vitamin kibao; zifuatazo ni sababu zinazokufanya ule matunda
kila siku:
AVOCADO:
Tunda hili limekuwa maarufu sana kwa kutengenezewa juice, lakini huenda
watu wakawa hawalipendi kwasababu ya kutokuwa na sukari katika radha
yake. Tunda hili linavitamini kibao, ambapo pia huongeza mafuta mwilini,
kwa wale walitumialo mara kwa mara.Unashauriwa kula au kunywa juice ya
avocado wakati wowote endapo kama huna matatizo yoyote yanayohusiana na
kuzidi kwa mafuta mwilini.Pia tunda hili huongeza uzito endapo
utalitumia mara kwa mara.
APPLE:
Hili ni tunda maarufu sana duniani lihusishwalo na wapendanao, lakini
tunda hili pamoja na kupewa umaarufu mkubwa duniani na kuwa na vitamini
na madini kibao, pia lina kazi kubwa sana katika kukupa muonekano mzuri
wa ngozi ya mwili wako.Tunda hili husaidia kuboresha mzunguko wa damu
mwilini pamoja na kuhifadhi ngozi isipoteze uhalisia wake.
NDIZI:
Hili pia ni tunda lenyejina kubwa kwa watu wengi wanaojali ulaji wa
matunda, kwani nitamu na lenye ladha safi.Tunda hili husaidia kulainisha
ngozi ya uso iliyokauka, kwa mfano utakuta kuna baadhi ya mafuta au
losheni zimecholwa ndizi.Kula ndizi ili urekebishe ngozi ya uso wako
pamoja na kuupa uwezo mzuri wa ukumeng'enya chakula.
PAPAI:
Ni tunda sahihi kabisa katika kukupa ngozi yenye mafuta, kurudishia au
kuziba sehemu zilizoumia na kunyofoka katika ngozi yako. Papai pia
hunga'arisha rangi ya ngozi yako, yote haya hufanyika na enzyme
inayotokana papai ambayo huitwa papain. Endapo kama unataka kutumia
papai katika ngozi yako ya uso, basi chukua asali changanya na papai
lililo iva na paka usoni kwako kwa dakika 10 kisha safisha, kisha utaona
kitakachotokea katika uso wako, utaonekana kama ngozi ya mtoto wa siku
mbili.
CHUNGWA:
Hili ni chungwa maarufu sana linalosaidia kurudishia ngozi iliyodhurika
na kuupa uhalisia wa ngozi yako. Jinsi ya kutumia ni rahisi sana,
chukua juisi ya chungwa ya baridi kisha paka usoni, acha kwa dakika 10
kisha osha utaona matokeo yake.
0 comments:
Post a Comment