Thursday 16 April 2015

MKURUGENZI SUMATRA ATOA TAMKO KUHUSU NAULI ZA MABASI NA DARADALA

Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Gillian Ngewe (kushoto) akitoa tamko, kulia kwake ni Eng. Dr. Michael Kisaka mwongozaji wa Reli nchini.
Mkurugenzi huyo (kushoto) akitoa ufafanuzi.
Viongozi hao wakisikiliza maswali kutoka kwa wanahabri(pichani hawapo).
MKURUGEZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA)ametoa tamko kuhusiana na nauli elekezi ya mabasi ya masafa marefu na mijini.
Akizungumza na wanahabari katika ofisi zao jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi huyo Gilliad Ngewe alisema mwishoni mwa mwaka 2014, mafuta yatumikayo katika vyombo vya usafiri wa abiria nchini yalianza kushuka hivyo mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra)ilikuwa ikipokea wito wa kupitia upya viwango vya juu vya nauli.
Alisema kuwa viwango hivyo vilikuwa vimewekwa na mamlaka Aprili 2013 na hivyo SUMATRA ikaamua kuandaa mikutano ya wadau kwa lengo la kukusanya maoni kuhusu haja ya kurekebisha viwango vya nauli zilizopo.
Aidha alisema kuwa mnamo Machi mwaka huu baraza la ushauri la watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na Sumatra liliwasilisha kwa Mamlaka ya Udhibiti na Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) maombi ya kushusha nauli za mabasi ya masafa marefu na mijini ambapo baraza liliainisha sababu za kuomba punguzo hilo kuwa ni kutokana na kushuka kwa bei za mafuta na kodi ya forodha kutoka asilimia 25 hadi punguzo la asilimia 10 kuanzia Julai 2014.
Ngewe alieleza namna walivyokubaliana na Bodi baada ya kutafakari viwango vilivyotokana na ukokotoaji uliozingatia masuala muhimu ili kukidhi matakwa ya watumiaji wa vyombo vya usafiri hivyo bodi iliridhia viwango vya nauli vilivyopo kuendelea kutumika kama kawaida kutokana na sababu iliyopelekea kubaki hapo ikiwa mojawapo ni usumbufu wa kurudisha chenji kutoka 376.77 iliyokuwa imekokotolewa ikiwa na punguzo la asilimia 5.8 hivyo nauli kubakia sh.400 za daladala.
Vilevile alieleza namna Bodi ilivyoamua kuwa nauli za mabasi ya hadhi ya juu (Luxury bus) kuwa hazitadhibitiwa ili kuchochea ubunifu katika utoaji huduma na ushindani kati ya huduma za barabara na njia nyinginezo za usafiri na katika viwango hivyo vipya vinapatikana katika tovuti ya mamlaka ambayo ni www.sumatra.go.tz.
Katika ufafanuzi wa viwango vipya vya mabasi ya masafa marefu, Ngewe alisema kuwa kutakuwa na jumla ya madaraja manne ambayo ni daraja la kawaida la chini barabara ya Lami 36.89 ya sasa ikiwa viwango vipya ni 34.00, punguzo ikiwa asilimia7.8, daraja la kawaida la chini barabara ya vumbi vya sasa ni 46.11 vipya ikiwa ni 42.50 sawa na asilimia 7.8, daraja la kawaida la juu 44.96 pamoja na daraja la kati la (Semi –Luxury bus) nauli ya sasa 53.22 nauli mpya ikiwa ni 50.13 sawa na punguzo la asilimia 5.81.
Alihitimisha kwa kusema kuwa viwango hivyo vya mabasi vinatarajia kuanza Aprili 30 mwaka huu na kuwaomba abiria wote kwa ujumla kutoa taarifa kwa SUMATRA endapo watatozwa zaidi ya nauli elekezi kuanzia siku hiyo kwa kupiga simu za bure ambazo ni 0800110019 au 0800110020.
PICHA/STORI NA DENIS MTIMA/GPL

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA