Thursday 16 April 2015

UEFA!! BAYERN HOI KWA FC PORTO ,YAPIGWA 3-1

FC Porto imeonyesha imepania kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuichapa Bayern Munich kwa mabao 3-1.



FC Porto ikiwa nyumbani imefanikiwa kuonyesha soka safi na kuwapa wakati mgumu  Munich walioambulia kipigo hicho.

Hata hivyo, Porto watalazimika kusubiri mchezo wa marudiano jijini Munich ili kujihakikishia nafasi ya kwenda nusu fainali.

Katika mechi hiyo kila timu ilicheza kwa kasi na kushambulia, lakini Porto ndiyo walizitumia nafasi zaidi kupitia kwa Ricardo Quaresma aliyefunga mabao mawili na Martnez akafunga moja huku Yhiago Alcantara akifunga bao pekee la Munich.



0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA