Sunday, 19 April 2015

UBAGUZI AFRIKA KUSINI: SOMA HAPA KILICHOWAKUTA RAIA WA AFRIKA KUSINI WAISHIO ZIMBWABWE

Licha ya Rais Jacob Zuma kulaani vurugu zinazoendelea Afrika Kusini dhidi ya wageni vurugu hizo zimezidi kupamba moto na kuvuka mipaka ya nchi hiyo,

Raia wa Afrika Kusini wanaoishi n akufanya biashara katika nchi za Msumbiji na Zimbabwe nao wameanza kushambuliwa ambapo malori yenye namba za usajili za Afrika Kusini yameshambuliwa Msumbiji, huku wanafunzi wa Vyuo vikuu Zimbabwe nao wakiandamana na kufanya fujo kwa wafanyabiashara na wawekezaji waliopo nchini humo.

Balozi wa Tanzania aliyeko Afrika Kusini amesema kuwa hakuna Mtanzania aliyeshambuliwa wala kuathirika na vurugu hizo.

Mmoja wa Watanzania ambao wanaishi karibu na mpaka wa Afrika Kusini na Msumbiji amesema malori zaidi ya 100 yanayosafirisha makaa ya mawe yamekwama baada ya mpaka kufungwa.
Toa Maoni Yako

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA