Saturday 9 May 2015

MVUA DAR ES SALAAM,CHEMBA ZA MAJI TAKA ZAPATA PAKUPONEA


Moja wapo ya mtaa uliopo maeneo ya Survey (savei) ukiwa umesheheni dimbwi la maji taka
Na Dickson Mulashani
Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam,baadhi ya wakazi wameshindwa kuwa wastaarabu na kufungulia chemba za maji taka(ya chooni) na kusambaa mitaani hali inayababisha kero kwa wapita njia pamoja na kuweka afya za  wakazi wa maeneo hayo katika hatari ya kuambikizwa magonjwa ya mlipuko.
Akipita katika baadhi ya mitaa ya survey mwandishi wetu alijionea adha hii na huku akishtushwa na hali  ya wenyeji wa eneo hili kwa kuonesha kuzoea uharibifu huu.
Mkazi wa Survey akijaribu kukwepa maji hayo kwa kutengeneza njia yake binafsi

Akizungumza na Funguka Live (kwa masharti ya kutupigwa picha ) mmoja wa mkazi wa eneo hili bwana Hamisi alieleza kuwa tabia hii imeshajenga mazoea hivyo wao kama wakazi hawana budi kulichukulia kama lilivyo.
Funguka Live ilichimba ndani zaidi kujua kiini cha mchezo huu na kubaini kuwa licha ya wengi kuwa na hali duni ya kugharamia gari la maji taka,baadhi wamejenga mazoea  ya tabia hii hivyo kuwa vigumu kuiacha.



Juhudi za kuwasiliana na Kiongozi wa eneo hilo pamoja na mtaalamu wa afya ziligonga mwamba kutokana na hali ya hewa na wingi wa maji katika njia mtaani hapo,Sambamba na hilo Funguka Live inatoa wito kwa watu wanaofanya mchezo huu kuacha mara moja kwani licha ya kutokuwa ya kiungwana pia inahatarisha afya zao.


Vile vile mtandao huu unaiomba seriali kupitia wizara ya afya kufuatilia suala hili na kuweza kulitafutia ufumbuzi kwani ni hatari.
Maji taka yakijitawala katika mtaa wa Pius Msekwa maeneo ya Survey


0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA