Saturday 16 May 2015

RAIS WA BURUNDI PIERRE NKURUNZIZA AREJEA NYUMBANI


Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza akirejea nchini mwake baada kushindikana kwa jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali yake alipokuwa nchini Tanzania kuhudhuria kikao cha viongozi wa EAC.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amejerea nyumbani hapo jana, baada ya kuwepo kwa jaribio la kumpindua akiwa nchini Tanzania kuhudhuria kikao cha viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokuwa wakijadili mgogoro wa Burundi. 
Maafisa wa serikali wanasema kurejea nyumbani kwa Rais huyo sasa ni ishara kuwa jaribio la kumpindua limeshindikana.
Wakati huo huo Mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Niyongabo amesema vikosi vya serikali ya Burundi vimefanikiwa kudhibiti hali ya mambo na kuzima jaribio la kumpindua Rais Pierre Nkurunziza. 

Tayari vikosi vya serikali vimetia nguvuni baadhi ya wanajeshi waliokuwa wakijaribu kuipundua serikali huku baadhi yao wakijitetea kuwa walirubuniwa. 
Hapo jana kulikuwa na mapigano makali karibu na radio ya taifa kati ya majeshi yaliyojaribu kuipindua serikali na yale yanayomtii Rais Pierre Nkuruziza.
-BBC SWAHILI

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA