|
Afisa msajili wilaya ya Moshi Bwana Mtugani Brighton akisoma baadhi ya maelekezo yaliyomo katika fomu ya kujiandikisha |
Semina ya uandikishwaji wa
vitambulisho vya uraia iliyoendeshwa na tume ya vitambulisho vya uraia nchini
NIDA imefanyika alhamisi hii katika chuo kikuu cha kumbu kumbu ya Stefano Moshi kampasi ya
mjini kilichopo manispaa ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.
Akiwa mzungumzaji mkuu katika
semina hiyo afisa msajili wilaya ya
Moshi Bwana Mtugani Brighton alianza kwa
kueleza faida za mwananchi kujiandikisha ili kupata kitambulisho cha uraia
pamoja na kutaja sifa za anaeweza kujiandikisha ili kupata kitambulisho hicho.
|
Bwana Mtugani Brighton akielezea jambo fulani katika semina hiyo |
“Ninyi wasomi,tunatazamia muwe
mfano wa kuigwa na jamii katika zoezi hili na kwa kutambua umuhimu huo tumeamua
kutembelea vyuo (vyote nchini) kwanza kabisa kutoa elimu na pili kuendesha
zoezi zima la uandikishwaji” alisema bwana Mtugani.
|
Mwanafunzi chuo kikuu cha kumbu kumbu ya Stefano Moshi kampasi ya mjini ndugu Hamis Faki akiuliza swali katika semina hiyo |
Katika semina hiyo ambayo
iliyohudhuriwa situ na wanafunzi pekee bali na uongozi, waadhiri pamoja na waajiriwa
wengine chuoni hapo elimu namna ya
kujiandikisha kuanzia hatua ya kwanza hadi ya mwisho ilitolewa huku
wahudhuriaji wakipata nafasi ya kuuliza maswali pale walipokuwa na uhitaji wa
maelezo ya ziada huku hofu kubwa ikiwa ni ucheleweshaji wa upatikanaji wa kitambulisho
hicho.
|
Mhadhiri wa chuo chuo kikuu cha kumbu kumbu ya Stefano Moshi Dr.Gasper Mpehongwa naye alihudhuria semina hiyo kupata elimu juu ya zoezi la uandikishwaji na namna ya kupata vitambulisho vya uraia
|
Mhadhiri wa chuo kikuu cha kumbu kumbu ya Stefano Moshi Ndugu C Z Mushi (mwenye kofia) akisikiliza maelezo katika semina hiyo |
|
Akitilia mkazo umuhimu wa zoezi
hili na kuwaondoa hofu akiahidi kutochelewa kwa vitambulisho hivyo,bwana
Mtugani alitoa wito kwa wanafunzi pamoja na wote waliohudhuria kuwa mabalozi wa
ujumbe huu kwa njia itakayoshawishi na wengine kujiandikisha na kujiepusha na
uvumi unaoenea kuwa serikali imeshindwa kuendesha zoezi hili.
Wakizungumza na mtanadao huu
baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho walieleza kuwa wameupokea ujumbe huo na
wapotayari kuutekeleza kwa matendo.
Picha,Habari na Dickson Mulashani
0 comments:
Post a Comment