WanaHabari Tuheshimiwe : Umoja wa Ulaya,UN Tutapigania Uhuru wa Habari Siku Zote
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika maadhimisho ya Uhuru wa habari duniani yaliyofanyika mkoani Morogoro. |
Na Joachim Mushi, Morogoro
UMOJA wa
Nchi za Ulaya nchini Tanzania (EU) umepinga vikali vitendo vya kikatili
na unyanyasaji wameokuwa wakifanyiwa na vyombo vya dola vya Serikali
wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ambapo ilitokea mwanahabari mmoja
kuuwawa. Alisema hawatachoka kukemea matukio hayo ya unyanyasaji kwani
yanafifisha uhuru wa habari.
Akizungumza mjini Morogoro katika Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Duniani, Kiongozi Mkuu wa Mabalozi hao, Balozi Filiberto Cerianse
Bregondi alisema EU itaendelea kupinga namna yoyote ya unyanyasaji kwa
wanahabari makundi yote wakiwemo wa mitandao ya kijamii hadi utakapo
kuwepo uhuru kamili wa vyombo vya habari. "...Tulifanya hivyo kwa mauaji
yalipotokea na tutaendelea kufanya hivyo siku zote watakapo kamatwa na
kupigwa wakiwa kazini...Tunajua huenda haitoshi lakini hii ni kutokana
na tofauti mbalimbali za kiutendaji," alisema Balozi Cerianse Bregondi.
Alisema
kupinga unyanyasaji kwa wanahabari haina maana wanachoandika wanahabari
mara zote ni cha kweli lakini ipo namna nzuri ya kushughulikia mvutano
kama huo na kusaidia kupata taarifa za kina zaidi zitakazofikia muafaka.
Aidha kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alisema
Tanzania inaongoza Afrika kwa kushindwa kuweka utaratibu mzuri wa
udhibiti mawasiliano.
Alisema
vyombo vya habari ni muhimu katika taifa na hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu
wa Taifa unaotarajia kufanyika Oktoba, alisema vyombo vya habari
vinaweza kubomoa au kujenga taifa lolote. "...Waandishi ni watu muhimu
katika kudumisha demokrasia nchini hivyo kuna kila sababu ya kuendelea
kujifunza zaidi.
Maadhimisho
ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kitaifa yamefanyika mkoani
Morogoro na kuhudhuriwa na wanahabari mbalimbali, wakongwe, wadau anuai
wa vyombo vya habari huku yakiwa na kauli mbiu ya Usalama wa Vyombo vya
Habari katika Dijitali: Uhandishi Mzuri unaozingatia, Usawa wa Kijinsia
na faragha.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani..Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalon Kibanda akizungumza
katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani..Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene akizungumza katika maadhimio hayo..Kaimu
Meneja wa Uhuru FM, Angela Akilimali (kulia) pamoja na wadau wa vyombo
vya habari katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani..Kutoka
kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Habari Umoja wa Ulaya, Susane Mbise na
Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu
akifuatilia mijadala katika mkutano huo..Mwanahabari na Bloga, Majid Mjengwa akizungumza katika mkutano huo.Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Mello akizungumza..Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
0 comments:
Post a Comment