BANZA STONE YUKO HOI, HAZUNGUMZI, AMEGOMA KULA CHAKULA NA KUNYWA DAWA, WASANII WENGI WAMEMTENGA – MAMA MZAZI
Mama mzazi wa muimbaji wa muziki wa dance, Banza Stone amesema mwanae afya yake imezidi kuzorota na sasa amegoma kula chakula wala kunywa dawa.
Akiongea na Ripoti ya kipindi cha Ubaoni cha EFM juzi, mama huyo alisema hadi siku hiyo Banza alikuwa amegoma kula kwa siku tatu mfululizo.
“Mpaka sasa sijamuona mtu yeyote aliyekuja kumshughulikia na kumwangalia, wamemwacha hivi hivi. Na mimi siwezi kuwalaumu kwanini hamjaja kumwangalia, kila mtu na moyo wake, mwenye kuja atakuja, mimi ntahangaika na mtoto wangu mpaka pale atakapoamua mwenyezi Mungu,” alisema Mama Banza.
Kwa mujibu wa kaka yake, Banza, Jabir Masanja, anasumbuliwa na fangasi kichwani mwake na dawa anazotumia ni kali kiasi cha kumpotezea hamu ya kula.
Jabir amewaomba wadau wa muziki na mashabiki wake walioguswa kumchangia chochote Banza kwa kutuma chochote kutumia namba: 0715407088 ,
0 comments:
Post a Comment