Wednesday 17 June 2015

DK SHEIN AISHUKURU CHINA KWA MISAADA


RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameishukuru Serikali ya China kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwaleta madaktari kila baada ya miaka miwili hapa nchini.
Dk Shein aliyasema hayo jana Ikulu mjini Zanzibar katika mazungumzo kati yake na madaktari 25 kutoka China waliomaliza muda wao wa kazi nchini waliofika Ikulu kwa ajili ya kumuaga Rais wakiongozwa na Balozi Mdogo wa nchi hiyo anayefanya kazi zake Zanzibar, Xie Yunliang.
Katika mazungumzo hayo, Dk Shein alisema utamaduni wa kuleta madaktari kutoka China ni wa kihistoria ulioanzia mwaka 1965 na umeendelea kuwepo.
Dk Shein alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wake wanathamini na wanazipenda huduma mbalimbali zinazotolewa na madaktari hao.
Pamoja na hayo, Dk Shein alitoa pongezi zake kwa Serikali ya China chini ya Rais Xie Jingping kwa kuendelea kuisaidia Zanzibar katika miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, Ujenzi wa Uwanja wa Mao tse Tung na ujenzi wa jengo jipya la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amaan Karume Zanzibar.
Kiongozi wa madaktari hao 25, Dk Liu Yaping akitoa shukurani kwa niaba ya madaktari hao alisema wamefurahia mazingira ya kufanyia kazi nchini na ushirikiano walioupata kutoka kwa madaktari wazalendo wa Zanzibari kwa ujumla. 
(HABARI LEO)

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA