Sunday, 14 June 2015

ICC:Rais wa Sudan taabani Afrika Kusini


Mahakama moja nchini Afrika Kusini imetoa agizo la kumzuia rais wa Sudan Omar al Bashir kutoondoka nchini humo

Mahakama moja nchini Afrika Kusini imeamuru rais wa Sudan Omar al Bashir asiondoke nchini humo.
Mahakama hiyo imemuagiza kusalia Afrika Kusini hadi itakaposikiza kesi iliyowasilishwa mbele yake ya kuitaka iamrishe serikali ya Afrika Kusini kumtia mbarani iliawasilishwe mbele ya mahakama ya Uhalifu wa Kivita ya ICC iliyoko Hague Uholanzi.
Rais Al-Bashir yuko mjini Johannesburg, Afrika Kusini, kuhudhuria mkutano wa muungano wa nchi za Afrika ambao unaanza leo Jumapili anatafutwa na mahakama ya ICC kutokana na makosa ya kivita na mauaji ya halaiki.
Muungano wa Afrika umekiuka maombi kadha ya kuitaka imkamate al Bashir katika miaka ya awali.
Hata hivyo Afrika Kusini ambayo ni mwanachama wa ICC inawajibu wa kutekeleza amri za mahakama hiyo na hivyo inaweza kumtia mbaroni al Bashir.

ICC ilikuwa imeiagiza serikali ya Afrika Kusini kumkamata rais wa Sudan Omar Al-Bashir.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC ilikuwa imeiagiza serikali ya Afrika Kusini kumkamata rais wa Sudan Omar Al-Bashir.
Kwenye taarifa yake , ICC ilisema kuwa waranti mbili za kumkamata Bashir bado zipo.
Rais al Bashir anatafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita kuhusiana na uhalifu ulitokea katika jimbo la Darfur na anakabiliwa na kesi inayohusiana na uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki.
-BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA