ROBERTO CARLOS AKITUPIA MBILI,REAL MADRID (LEGENDS) IKIICHAKAZA LIVERPOOL (LEGENDS) 4-2
Harry Kewell ndio alikuwa wa kwanza kufunga kwa upande wa Liverpool mnamo Dakika ya 18 ya mchezo kwa kupiga kichwa safi wakati akipokea krosi. Micheal Owen alikuwa mchezaji wa Pili kupachika Bao kwa kupiga Kichwa safi kilichomshinda mlinda lango wa Real Madrid na kutinga wavuni na kuandika Bao la Pili la kuongoza kwa Liverpool.
Timu ya Real Madrid ilitoka nyuma na kuibuka mshindi wa Mechi hiyo kwa jumla ya Magoli 4-2 katika Uwanja wa Santiago Bernabeu jumapili ya leo.
Real waliweza kupata penalt ambayo ilipigwa na mkonge Roberto Carlos mnamo dakika ya 43 na kuiandikia Real Madrid goli la Kwanza, Hadi mapumziko Liverpool walikuwa wanaongoza kwa matokeo ya 1-2.
Kipindi cha Pili kilianza kwa Real madrid kufanya mashambulizi mengizaidi na kuweza kuzaa matunda mnamo dakika ya 52 waliweza kupata penalt ya pili na kupigwa na yule yule mkongwe R.Carlos na kuandika goli la pili la kusawazisha.
Hali ilizidi kuwaelemea Liverpool kwani waliruhusu mashambulizi langoni kwao na mnamo dakika ya 68 Amavisca aliweza kuipatia Bao la Tatu Timu yake ya Real Madrid goli la Kuongoza, Dakika ya 83 Perez alifunga kalamu ya magoli kwa kupachika Goli la nne kwa Real Madrid na Hadi mwisho wa Mchezo Matokeo yalibakia 4-2.
Harry Kewell katika Picha akimkabili Michel Salgado, katika mechi dhidi ya Magwiji wa Real Madrid pale Santiago Bernabeu
Gwiji wa soka Zinedine Zidane alikuwa mmoja wa Wachezaji walioipa Ushindi dhidi ya Wenzao wa Liverpool.
VIKOSI: Real Madrid Legends XI: Buyo, Salgado, Carlos, Sanchis, Zidane, Morientes, Seedorf, Karembeu, Sanz, Solari, Makelele.
Subs: Contreras, Rojas, Garcia Cortes, Pavon, Sabido, Congo, Butragueno, Perez, Velasco, Amavisca.
Goals: Carlos 43 pen, 52 pen, Amavisca 68, Perez 83
Liverpool Legends XI: Dudek; McAteer, Carragher, Kvarme, Harkness; Garcia, McNanaman, Berger; Fowler; Owen, Kewell.
Subs: Westerveld, Jones, Thompson, Xavier, Smicer, Diao, Henchoz, Rush, Partridge.
Goals: Kewell 18, Owen 21
0 comments:
Post a Comment