MANCHESTER UNITED (LEGENDS) YAINYUKA BUYERN MUNICH (LEGENDS) 4-2 OLD TRAFFORD,
Kwenye Mechi ya Hisani iliyochezwa hii Leo huko Old Trafford, Malejendari wa Manchester United wamewatwanga wenzao waBayern Munich Bao 4-2 mbele ya Mashabiki 50,128.Mwaka Jana kwenye Mechi kama hii iliyochezwa huko Allianz Arena Jijini Munich, Timu hizi zilitoka Sare ya 3-3.
Katika Mechi ya Leo, Mabao ya Man United yalifungwa na Louis Saha, Dakika ya 9, Dwight Yorke, 39, Andy Cole, 45, naJesper Blomqvist, 83, wakati yale ya Bayern yalifungwa na Zickler , Dakika ya16, na Tarnat, 42.
Paul Scholes akiongea na Gwiji wa Buyern Munich alipoiongoza Manchester United kama Captain leo hii Old Traford.
Magwiji wa Manchester United J.S.Park, Cole na Yorke wakishangilia moja ya Goli katika mchezo huo wa Magwiji wa Manchester United na Buyern Munich, Pale Old Traford
Magwiji wa Buyern Munich wakishangilia moja ya Goli katika mchezo wao dhidi ya Mancheste United leo hii pale Old Traford
Hakika bado yupo fiti Ji Su Park akionesha Skils zake katika Utulizaji wa Mpira
VIKOSI: MAN UNITED: Van der Sar (van der Gouw 61); P.Neville (Martin 77), Johnsen (Dublin 40), Stam, Irwin (Silvestre 40); Fortune (Blackmore 77), Park (Poborsky 46), Scholes (Thornley 77); Yorke (Beardsmore 77), Saha (Blomqvist 17), Cole (Ritchie 67).
BAYERN MUNICH: Butt; Jorginho (Sternkopf 69), van Buyten, R.Kovac (Witeczek 46), Pflugler (Kreuzer); van Bommel (Gaudino 46), Breitner (Tarnat 20, Rummenigge 61), N.Kovac (Schupp 46, Breitner 78), Paulo Sergio; Zickler, Makaay (Zimmermann 69)
0 comments:
Post a Comment