Monday, 29 June 2015

WATOTO MILIONI 6.3 HUFARIKI DUNIA KILA MWAKA

 Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini, Rabikira Mushi akizungumza katika mkutano wa afya na haki za binadamu katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (kushoto) ni Mwakilishi wa Ofisi ya Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa,Bi.Joyoti Sanghera.
Na Bakari Issa.
WATOTO Milioni 6.3 wa chini ya miaka mitano hufariki dunia kila mwaka duniani kote kutokana na kutokuwa na uangalizi bora wa afya kwa watoto hao, huku asilimia 95 ya vifo hivyo hutokea katika Bara la Afrika na Asia.
Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa Ofisi ya Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa,Bi.Joyoti Sanghera wakati akizungumza na wadau wa afya na haki za binadamu katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Katika kupambana na changamoto za vifo vya watoto,Ofisi ya Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na UNCT nchini Tanzania pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini wameandaa mkutano utakaoshauriana juu ya misingi ya Haki za Binadamu katika kupunguza vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Sanghera amesema Ofisi ya Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa iko tayari kusaidia haki za watoto ili kuondokana na tatizo la afya na vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano linaloikabili dunia.
Kwa upande wake,Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini, Rabikira Mushi amesema vifo vya mama na watoto hutokea hapa nchini kutokana na changamoto zinazoikabili nchi ikiwa ni miundombinu ya vituo vya Afya na kutokuwa na Wauguzi wenye kutoa elimu sahihi juu ya afya na uangalizi wa mtoto hususani vijijini.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA