Monday, 29 June 2015

IJUE NCHI ITAKAYO ANDAA CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP 2015

RAIS wa Shirikisho la Soka Ethiopia, Juneydi Basha, amethibitisha kuwa wataandaa michuano ya mwaka huu ya Kombe la Chalenji, baada ya Shirikisho la Soka la Rwanda (FERWAFA) kuipiga chini ofa hiyo.
Rwanda ilipewa fursa hiyo, lakini imeitosa na kuamua kuweka nguvu nyingi katika maandalizi ya michuano ya Afrika kwa Wachezaji (CHAN) mwakani ambayo ni wenyeji.
"Basha ametwiti katika ukurasa wake akisema: "Ethiopia itakuwa mwenyeji wa Kombe la Chalenji 2015. Ninawaomba tuunganishe nguvu zetu kufanikisha michuano hii. Hongereni kwa fursa hii."
Kenya ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kushinda jijini Nairobi 2013. Michuano hiyo haikufanyika mwaka jana baada ya waliokuwa wamepewa uenyeji, Ethiopia, kujitoa dakika za mwisho.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA