|
Mwenyekiti wa MALIHAI chuo kikuu cha kumbukumbu ya Stefano Moshi David Kaganda akimkabidhi cheti mwanachama katika campus ya Mwika |
Zoezi hilo lililofanyika katika campus mbili tofauti za chuo hicho kilichopo mkoani Kilimanjaro ikiwa ni Masoka pamoja na Mwika liliendeshwa na viongozi wa chama hicho cha watunza mazingira nchini Tanzania.
Akisimamia zoezi hilo katika campus ya Mwika ,mwenyekiti wa MALIHAI chuoni hapo
David Kaganda aliambatana na rais mteule wa chuo hicho Filbert Mafuta ambapo waligawa vyeti hivyo kwa wanachama wa mwaka wa tatu wanaotarajia kuhitimu masomo mwezi ujao.
Zifuatazo ni picha za tukio hilo katika campus ya Mwika.
|
Mwenyekiti wa MALIHAI David Kaganda akiwasilisha ripoti fupi ya mwenendo wa Chama mbele ya waliohudhuria zoezi hilo |
|
Wanachama wa MALIHAI campus ya MWIKA waliohudhuria zoezi hilo wakimsikiliza Mwenyekiti wao |
|
Mwenyekiti wa MALIHAI David Kaganda (wakwanza kushoto) Samwel Mwakeja aneafuata ,Rais wa Serikali ya wanafunzi Filbert Mafuta (aliyevaa Suti) wakiwa katika picha ya pamoja |
|
Wanafunzi waliokabidhiwa vyeti katika picha ya pamoja na viongozi wa MALIHAI |
|
Viongozi wa MALIHAI na wale wa Serikali ya wanafunzi chuoni hapo katika picha ya pamoja |
Picha na Abdul Hakim Hilal
0 comments:
Post a Comment