Saturday, 27 June 2015

OSPINA AONESHA UBORA WAKE LAKINI ARGENTINA YATINGA NUSU FAINALI KWA MIKWAJU YA PENATI,


ArgentinaMkwaju wa penati wa Carlos Tevez umeipeleka Argentina kwenye hatua ya nusu fainali ikiitupa nje timu ya taifa ya Colombia kwenye mchezo wa  robo fainali ya aina yake kuwahi kutokea kwenye historia ya michuano ya Copa America na kuufanya mchezo huo kuvuta hisia za watu wengi tofauti kwenye mashindano yanayoendelea huko nchini Chile.

OspinaGolikipa wa Arsenal na timu ya taifa ya Colombia David Ospina akiwa katika ubora wa hali ya juu aliweza kuokoa michomo kadhaa ya Lionel Messi na Sergio Aguero na kuifanya timu yake kuwa salama muda wote wa mchezo kwenye mhezo ambao ilibidi ungezewe dakika 30 za ziada baada ya kumalizika kwa dakika 90 za kawaida ili kumtafuta bingwa wa robo fainali hiyo ngumu atakae tinga hatua ya nusu fainali.

Ospina 1Haikuwa kazi rahisi kwa Argenina kupata goli mbele ya Colombia japo walitawala mechi hiyo ya robo fainali na ilibidi matuta pekee ndio yaamuwe ni timu ipi kati ya hizo mbili itasonga mbele kwa hatua inayofuata (nusu fainali).
Tevez aliyeingia dakika ya 73 kuchua nafasi ya Aguero akaibuka shujaa kwa upande wa Argetina kwa kufunga penati yake ikiwa ni penati ya 14 kupigwa kwenye mchezo huo na kuipa Argentina nafasi ya kucheza nusu fainali kwa ushindi wa penati 5-4.
MessiArgentina inasubiri kucheza nusu fainali na mshindi wa mechi ya usiku wa leo kati ya Brazil dhidi ya Paraguay ambapo mchezo wa nusu fainali kati ya Argentina na mshindi kati ya Brazil na Paraguay unatarajiwa kupigwa Jumanne ijayo.
Ospina 2Baada ya dakika 120 za mchezo kumalizika ndipo mikwaju ya penati ikatumika kumpata mshindi, zilipigwa penati 14 ili kumpata mshindi wa mchezo huo. Penati zilikuwa kama ifuatavyo;
1 Rodriguez – 1-0 Colombia 
2 Messi – 1-1
3 Falcao – 2-1 Colombia 
4 Garay – 2-2
5 Cuadrado – 3-2 Colombia 
6 Banega – 3-3
7 Muriel – 3-3 
8 Lavezzi – 3-4 Argentina 
9 Cardona – 4-4
10 Biglia – 4-4
11 Zuniga – 4-4 
12 Rojo – 4-4
13 Murillo -4-4 
14 Tevez – 5-4
Argentina ikatinga nusu fainali kwa ushindi wa penati 5-4 nakuisukumiza nje ya mashindano timu ya Colombia.
Argentina 1

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA