Tuesday 11 August 2015

MANCHESTER CITY YAFUNGUA PAZIA LALIGI KWA KUITANDIKA WEST BROM GOLI 3 BILA


Yaya Toure ameanza vyema ligi kuu nchini England kwa kuonyesha makali yake, pale alipofunga mara mbili na kuisaidia timu yake ya Manchester City kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya West Brom, mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo. 

Katika mchezo huo, West Brom waliokuwa katika uwanja wao wa nyumbani walishindwa kabisa kuzuia mashambulizi ya washambuliaji wa Manchester City waliokuwa na hamu ya kufumania nyavu na kuanza vyema ligi hiyo.
Mbali ya Yaya Toure kufunga mabao mawili katika dakika za 9 na 24 dhidi ya matatu ya timu yake, pia nahodha wa timu hiyo Vicent Kompany alifunga bao la tatu nala ushindi katika dakika ya 59.


Yaya Toure akipiga shuti kali lililo zaa bao la pili
Sagna akimpongeza Yaya Toure baada ya kupachika bao




0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA