Sunday 30 August 2015

REAL MADRID YAFANAYA MAUAJI WAKATI BALE NA JAMES WAKICHEKA NA NYAVU MARA MBILI


Gareth Bale na James Rodriguez wameifungia Real Madrid magoli mawili kila mmoja wakati timu hiyo ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Real Betis katika ligi ya La Liga.

Katika mchezo huo Gareth Bale aliifungia Real Madrid bao la kwanza mnamo dakika ya pili tu ya mchezo kwa kuunganisha kwa kichwa mpira wa krosi uliopigwa na James Rodriguez.

Kipa wa Real Madrid Navas alionekana kuwa shujaa mpya baada kuokoa mchomo katika kipindi cha kwanza na pia katika kipindi cha pili alipomnyima bao Ruben Castro.
            Gareth Bale akipiga mpira wa kichwa uliotinga wavuni na kuandika bao la kwanza
                                                    James Rodriguez akipiga shuti lililotinga wavuni 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA