BURKINA FASO: RAIS NA WAZIRI MKUU WASHIKILIWA NA JESHI
Rais wa Burkina Faso Michel Kafando (kushoto) Na Luteni Kanali Isaac Zida, katika sherehe ya kupeana madaraka, Novemba 2014, Ouagadougou.
Na RFI
Wanajeshi kutoka kikosi cha usalam wa Rais wanamshikilia tangu Jumatano mchana wiki hii Rais wa Burkina Faso, Waziri Mkuu Isaac Zida pamoja na mawaziri kadhaa, baada ya kuingia ghafla katika Ikulu wakati wa kikao cha Baraza la mawaziri mjini Ouagadougou.
Hali bado ni tata katika Ikulu ya Kosyam , makao makuu ya Ofisi ya Rais mjini Ouagadogou. Jeshilimezingira maeneo hayo Jumatano Jioni wiki hii. Wanajeshi hao ni pamoja na wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa taasisi mbalimbali za uongozi wa nchi (RSP), ambao waliingia wakati wa kikao cha Baraza la mawaziri. Wanajeshi hao wamewapokonya silaha askari waliokua wakitoa ulinzi katika maeneo hayo, na kuwapokonya simu za mawaziri waliokua nazo na baadaye walifunga lango la Ikulu.
Kwa sasa, ni vigumu kujua nini kinaendelea ndani majengo hayo. Rais wa mpito, Michel Kafando na Waziri Mkuu Isaac Zida na Mawaziri kadhaa wa serikaliwako mikononi mwa wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa taasisi za uongozi wa nchi. Hakuna madai hadi sasa ambayo yametolewa na kundi hili la wanajeshi.
Mahusiano si mazuri kati ya Waziri Mkuu Isaac Zida, kutoka jeshi, na wanajeshi wa Kikosi cha usalama wa Rais. Migogoro mingi - mwezi Desemba, Februari na Juni - ilitokea kati ya Isaac Zida marafiki zake wa zamani. Na kuingilia kijeshi kwa wanajeshi hao kunakuja wakati ambapo Jumatatu wiki hii, tume ya maridhiano na mageuzi iliyoteuliwa katika kipindi cha mpito ilitoa ripoti yake, ambayo inataka hasa kuvunjwa kwa kikosi cha usalama wa rais (RSP). Je, kuna uhusiano ya moja kwa moja kati ya matukio haya? Kwa sasa, bado ni vigumu kusema kwani madai ya askari wanawashikilia viongozi hao hayajulikani.
Kuingilia huko kwa wanajeshi wa RSPpia kunakuja wiki chache kabla ya uchaguzi wa rais na wabunge, uliyopangwa kufanyika Oktoba 11 kama sehemu ya mchakato wa mpito, ambayo ilianza baada ya kuanguka kwa utawala wa Blaise Compaoré, Oktoba 31 mwaka 2014, baada ya miaka 27 akiwa madarakani.
0 comments:
Post a Comment