Friday 11 September 2015

Mnara wa Mau Mau kuzinduliwa Nairobi



Mnara wa kumbukumbu wa Mau Mau

Mnara wa kuwakumbuka wapiganaji wa Mau Mau, walioongoza vita vya ukombozi kutoka kwa utawala wa kikoloni nchini Kenya, miaka ya 50, utazinduliwa rasmi hiyo kesho katika bustani ya Uhuru mjini Nairobi.
Waandalizi wa hafla hiyo tayari wametoa picha za mnara huo wa kumbukumbu.


Mnara wa kumbukumbu wa Mau Mau

Mnara huo umefadhilia na serikali ya Uingereza, kama sehemu ya mkataba ulioafikiwa mwaka wa 2013, ambao pia uliidhinisha wapiganaji hao kulipwa fidia ya £20m, kwa wapiganaji hao wa Mau Mau ambao walidhulumiwa na kuteswa na wanajeshi wa kikoloni wa Uingereza.

Image captionMnara wa kumbukumbu wa Mau Mau

Serikali ya Uingereza ilikubali kuwa Wakenya hao waliteswa na kuwa inajuta mateso na dhuluma waliyoyapata.
-BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA