Wednesday 16 September 2015

RONALDO APIGA HAT-TRICK, MADRID YAITUNGUA SHAKTHAR 4-0


Mshambuliaji Gareth Bale ameumia na kutolewa nje wakati Real Madrid ikipambana na Shaktar Donestik katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini hiyo haikuimzuia Cristiano Ronaldo kupiga tatu, hat trick na kuiwezesha Madrid kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0cikiwa nyumbani.

Katika mabao hayo matatu aliyofunga katika dakika za 55, 63 na 81, mawili yalikuwa ya mikwaju ya penalti.

Kwa ushindi huo, Madrid imepaa hadi kileleni mwa kundi ukiwa ndiyo mchezo wake wa kwanza msimu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Bao moja la Madrid lilifungwa na Karim Benzema, hata hivyo Madrid ilipoteza nafasi nyingi za kufunga.



0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA