Wednesday 7 October 2015

VIDEO::BOCCO ALIMPIGA TEKE NYOSSO KABLA HAJADHALILISHWA

Image result for nyosso na bocco

Na Dickson Mulashani,

Katika kipindi cha hivi karibuni jina la Juma Nyosso limetawala sana katika vyombo vya habari,mitandao ya kijamii na hata kuzagaa mitaani kufikia hatua ya kuzua hadi utani.
Wengi wakimlaumu wengine wakilaani kitendo alichokifanya na wengine kusema adhabu ya kufungiwa miaka miwili kutojihusisha na soka linalotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kuwa ni ndogo na alistahili kufungiwa kucheza soka kabisa (Binafsi sikubaliani na hilo).

Ni kweli kabisa kuwa alichokifanya Nyosso ni nje kabisa ya taratibu za mchezo soka.Tangu taarifa hii na picha za tukio liliposambaa kwenye mitandao na vyombo vya habari nilijiuliza sana ilikuwaje Nyosso atoke atokako na kumtenda vile Bocco? Naamini wengi hawakulitizama hilo ila wameegemea kumkosoa na kumuona fedhuli (Kwa upande fulani Nakubaliana nao).

Wakati hili likiendelea nimebahatika kuona sehemu ndogo ya tukio hilo na kubaini kuwa kulikuwa na rabsha uwanjani hapo miongoni mwa wachezaji Bocco kumpiga teke Nyosso ambapo alijibu mapigo kwa Uhuni ule.
Image result for nyosso na bocco

Sijabahatika kuona namna Nyosso alivyowatendea Elias Maguli na Amir Mafta pamoja na Joseph Kaniki kama inavyozungumzwa kuwa nao ni wahanga wa Uhuni huo wa Nyosso lakini ukweli unaothibitika kwa video hii ni kwamba BOCCO ALIMPIGA TEKE NYOSSO KABLA HAJADHALILISHWA japokuwa hilo halikuhalalisha na halihalalishi uhuni wa Nyosso.
Nimalize kwa kukemea vitendo vya kihuni katika soka hasa kwetu sisi ambao tupo katika mchakato wa kuliinua soka letu kwa kujenga viwango vya wachezaji wetu ili tuweze kuwika Afrika na duniani kwa ujumla nikikumbusha kuwa Nidhamu ndio nguzo inayobeba dhamana ya kipaji chochote kile.

Pongezi zangu ziwaendee TFF kwa kuliona hili na kumkanya Nyosso kwa kauli na pia adhabu kwani imeonesha kuwa "avunjaye mwiko hana budi kulala njaa".

Namtakie Nyosso maisha mema ya kutumikia adhabu yake nikiamini atakuwa amejifunza mengi vile vile nampe pole Bocco na kumtakia heri katika harakati zake za soka.
YA NYOSSO YAMEPITA SASA TUENDELEZE SOKA.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI  

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA