Wednesday 7 October 2015

ROGERS: NIMESIKITISHWA SANA KUONDOKA LIVERPOOL

rodstat
Kocha ambae ameachishwa kazi hivi karibuni na club ya Liverpool ametoa statement yake kupitia League Managers Association.
Stament hiyo inasomeka hivi, “Nimesikitishwa sana kwa kuondoka kwenye club ya Liverpool, ni furaha kwangu na najivunia kuiongoza club kubwa kama LIverpool kwa miaka 3 iliyopita. Nilifanya kazi kila siku kwa uwezo wangu wa juu ili kuwakilisha club vizuri, kuendeleza mchezaji mmoja mmoja na timu kwa ujumla. Kuna mambo mengi ya kujivunia na kukumbuka kwenye maisha yangu ndani ya club nikiwa na wachezaji wanaojituma sana. Kikosi kilichopo sasa hivi ni kipya lakini kina vipaji vya kutosha. Nawatakia wafanye vizuri kwenye siku zinazokuja wakiwa chini ya kocha atakae waongoza ndani ya siku zijazo.”
“Liverpool ina urithi na historia kubwa ya soka na sina kingine bali ni heshima juu ya hilo. Kuna vitu vya tofauti ambavyo vinafanya club na eneo la Liverpool kuwa very special. Ningependa kuwashukuru watu wote kwenye club hasa Fenway Sports Group, Liverpool directors, makocha nilikua nao kwenye benchi,wafanya kazi kwenye club, wachezaji na watu wote kwa muda ambao nimefanya kazi.”
“Pia ningependa kutoa asante maalim kwa John W. Henry, Tom Werner na Mike Gordon kwa kunipa nafasi ambayo ni nzuri kwenye historia ya maisha yangu ya soka na naamini urafiki utaendelea kwenye siku za mbeleni”

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA