KILI STARS YAITULIZA RWANDA, YAFUZU ROBO FAINALI CHALENJI, ZANZIBAR YALOA
Kilimanjaro Stars inayonolewa na Abdallah Kibadeni imefuzu hatua ya robo fainali baada
ya kuinyamazisha Rwanda kwa kuichapa kwa mabao 2-1.
Katika mechi hiyo iliyopigwa mjini Wassa, Stars
ilipata bao moja katika kila kipindi.
Bao la kwanza lilifungwa na Said Ndemla na la pili
likatupiwa na Simon Msuva katika kipindi cha pili baada ya kipa wa Rwanda
kufanya uzembe.
Stars imefikisha ponti sita baada ya kuifunga Somalia
kwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza.
Tayari ina nafasi ya kufuzu, kwani hata timu nyingine
katika kundi lake itafikisha pointi 6, bado itakuwa na nafasi, zikifikisha timu
mbili, bado itakuwa na nafasi ya best looser.
Mechi ya mwisho ya Kili Stars hatua ya makundi itakuwa
dhidi ya wenyeji Ethiopia walioanza michuano kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa
Rwanda.
Katika
mechi ya awali, Zanzibar Heroes ilitandikwa mabao 4-0 Uganda ambao
walianza michuano hiyo kwa kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Kenya.
0 comments:
Post a Comment